Share this Post

dailyvideo

Kipimo cha SCAN Muhimbili Chaharibika



Kipimo cha CT Scan (pichani) Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kimeharibika kwa muda wa miezi sita sasa hali inayosababisha usumbufu kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo na kuandikiwa kipimo hicho.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka hospitalini hapo, kimesema licha ya uongozi wa hospitali kuwa na taarifa hizo lakini hakuna juhudi zilizofanyika.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa, ukosefu wa kipimo hicho umesababisha wagonjwa kupata huduma hiyo nje ya hospitali na kuleta usumbufu. "Kinachoshangaza wiki iliyopita hospitali iliandaa bonanza la michezo linalogharimu kiasi cha milioni 15/- lililoshirikisha Kurugenzi mbalimbali lakini mambo ya muhimu kama haya imeshindwa kuyashughulikia," kimeeleza chanzo hicho na kuongeza:"Kifaa hicho kimeharibika kabla ya madaktari kugoma, tulifikiri kitashughulikiwa kwa wakati ili wagonjwa wanaofika hapa wapate huduma ndani ya hospitali yao ya umma lakini matokeo yake daktari anaandika vipimo kisha mgonjwa anaambiwa huduma hiyo haipo na kulazimika kwenda nje ya hospitali, hii ni aibu," chanzo hicho kimebainisha.

Kadhalika, kimeeleza kuwa, mara kwa mara mashine za hapo zimekuwa zikilalamikiwa kuharibika na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakiitegemea hospitali hiyo kama mkombozi wa maradhi yanayowasumbua.

Afisa Uhusiano wa hospitalini hapo, Aminiel Aligaesha, alipoulizwa kuhusiana na tatizo hilo kwa njia ya simu alisema kuwa yupo kwenye mkutano.

Januari mwaka huu gazeti hili liliandika habari kuhusu kuwepo kwa baadhi ya vipimo vikubwa ndani ya hospitali hiyo kushindwa kutolewa kutokana na vifaa vyake kuharibika huku baadhi ya dawa za kufanyia vipimo kutokuwepo.

Katika taarifa hiyo baadhi ya vipimo vilivyokuwa havifanyi kazi ni vile vya magonjwa yahusuyo upimaji wa damu kama figo, ini sukari, mafuta (CCP) na mengine havifanyiki kwa sababu dawa za kufanyia zimeisha.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa, karatasi (film) za vipimo vya MRI na CT Scan zilikuwa hazipo.

Kadhalika mapema mwezi uliopita NIPASHE ilipata taarifa kuwa mashine nyingine ambayo kazi yake ni kukata vinyama kwa ajili ya kupima ugonjwa wa kansa kwa mgonjwa pia imeharibika.


CHANZO: NIPASHE

Posted by Editor on 15:17. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Kipimo cha SCAN Muhimbili Chaharibika

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery