Share this Post

dailyvideo

Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Sothern Sudan katika mashindano ya Miss East Africa 2012







Miss Akuot Philip Suzan (20) katika pozi


Mrembo huyo ni  Miss Akuot Philip Suzan (20)  mwenye urefu wa futi 6.1 anaekaa Juba, Sudan  ni mwanamitindo Nchini humo na anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha makelele Nchini Uganda mwaka huu.

Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss Ayisha Nagudi (23) ambae ni mwakilishi wa Uganda.

Nchi zilizobaki zinaendelea
kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya
Miss East Africa 2012 ambayo yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu
ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi
zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja
na visiwa vya Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.

Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania.

Posted by Editor on 14:34. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Sothern Sudan katika mashindano ya Miss East Africa 2012

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery