Share this Post

dailyvideo

Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lamlilia Magoma Shaban



Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi
za Kulipwa Tanzania (TPBC) zinamlilia bingwa wa IBF wa mabara na bingwa
wa dunia wa WBU Magoma Shaban.

Magoma aliyefariki jana katika hospitali ya Bombo jijini Tanga atakumbukwa kwa umahiri wake kwenye ngumi za kulipwa.

Safari ya Magoma Shaban kwenye ngumi za kulipwa ilianzia katika
uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga mwaka 1998 wakati Onesmo Ngowi akiwa
ndio kwanza alipoteuliwa na Rais wa zamani wa IBF Robert Lee Sr toka
Marekani kuanzisha shirikisho hilo la IBF katika bara la Afrika.

Katika uwanja huo Magoma Shaban alipigana na Joseph Waweru toka
Kenya na kumshinda kwa KO na kutangazwa kuwa bingwa wa IBF katika bara
la Afrika uzito wa flyweight.

Mwaka 2000 Magoma chini ya kamouni ya Capital Promoters Limited
chuini ya mwandishi wa bahari mahiri bwana Gabriel Nderumaki alipigana
na bondia Totim Lukunim toka Thailand katika ukumbi wa PTA kugombea
mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Flyweight na kumshinda  kwa KO
katika raundi ya 4. Huo ndio ukawa mwanzo wa magoma Shaban kwenye kwenye
matawi ya juu katika ngumi.

Magoma Shaban alipigania ubingwa wa dunia wa WBU nchini Italy na kumshinda bondia Ferid Ben Jeddou kwa TKO katika raundi ya 6.

Magoma alikuwa ni bondia aliyeing'arisha Tanzania na bara zima la Afrika katika medani ya ngumi za kulipwa duniani.

Kwa mantiki hiyo leo IBF imetangaza rasmi kuuita mkanda wa uzito wa Fly aliokuwa anachezea Magoma kuwa "Mkanda wa Magoma Shaban" katika mapambano yote yatakayokuwa yanachezezwa katika uzito huu yatajulikana kama "Ubingwa wa IBF Africa wa Magoma Shaban".

Tunafanya hivi ili kuwaenzi mabondia wanaoleta mchango mkubwa
katika medani ya ngumi na hivyo majina yao kubakia katika kumbukumbu
zetu milele.

Mola alitoa na Mola ametwa, jina lake lihidimiwe milele. Amin!

Posted by Editor on 09:44. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lamlilia Magoma Shaban

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery