PICHA ZA WANAHABRI MBALI MBALI WALIOANDAMANA JIJINI DAR KULAANI MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI..
Mwanahabari akionyesha ishara ya kazi yao kunyimwa uhuru
Wengine walibeba picha ya marehemu Daudi Mwangosi
WANAHABARI jijini Dar es Salaam leo wameandamana kutoka Kituo Cha Televisheni cha Channel Ten na kuhitimisha maaandamano yao katika Viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kulaani mauji ya kikatili aliyofanyiwa mwandishi mwenzao, Daudi Mwangosi wa Kituo cha Chanel Ten mkoni Iringa. Katika Maandamo hayo Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emannuel Nchimbi alifika Viwanja vya Jangwani kupokea maandano hayo lakini alitimuliwa na wanahabari. Picha zaidi zinafuta kwa chini
Wanahabri wakiwa na mabango yenye ujumbe mbali mbali yakulaani mauaji ya Mwangosi na kutetea fani ya uandhisi na usalama wao wakiwa makazini
Wanahabari wakiandamana kuelekea Viwanja vya Jangwani leo asubuhi kulaani mauaji ya mwanahabari mwenzao, Daudi Mwangosi
Wanausalama pia walikuwepo kimya kimya kuhakikisha kuna usalama
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emannuel Nchimbi akiongea na wanahabari hao.
Waziri Nchimbi akiondoka baada ya kutimuliwa na waandhishi hao
(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)




