BINTI MWANAHARAKATI WA PAKISTAN ALIYEPIGWA RISASI KICWANI AWASILI UINGEREZA KWA MATIBABU.
Malala Yusoufzai.
Msichana wa Kipakistani aliyepigwa risasi kichwani wiki iliyopita kwa sababu ya kampeni yake kwa elimu ya wasichana Malala Yusoufzai, amewasili nchini Uingereza kupata matibabu.
Malala mwenye umri wa miaka 14 amewasili mjini Birmingham baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Pakistan kuondoa risasi mwilini mwake.
Madaktari wamesema itachukua muda mrefu kwa msichana huyo kuweza kupona majeraha ya kimwili na ya kisaikolojia.
Malala alipata umaarufu baada ya makala aliyoandika kwa ajili ya shirika la utangazaji la Uingereza, BBC, akielezea unyanyasaji unaofanywa na wanamgambo wa Taliban.
Watu wasiojulikana walisimamisha basi aliyokuwa akisafiria kutoka shule na kumpiga risasi.





