Diamond Platnumz kuachia ngoma mpya kesho

Diamond na Raqey wakichagua picha ya kutumia kwenye cover ya wimbo wake mpya
Baada ya miezi kadhaa ya ukimya bila track mpya hewani hatimaye staa wa ‘Mawazo’ Diamond Platnumz kesho anatarajia kuachia wimbo wake mpya.
Ngoma hiyo ameipa jina la ‘Nataka Kulewa’ ambayo imefanywa na producer wa AM Records, Manecky.
Kupitia website yake, Diamond ameshare kwa mashabiki wake picha za utengenezaji wa cover ya ngoma hiyo uliosiomiwa na Raqey Mohamed wa I-View Media kampuni ambayo inamsimamia.
Kuhusu mipango ya video aliyoifanyia usaili wa models wiki kadhaa zilizopita Raqey amesema bado wanashughulikia permit na hivi karibuni alikuwa Dubai kwaajili ya kuweka mambo sawa.
Raqey na Martin Kadinda
Raqey na wengine wakiangalia picha zilizopigwa
Diamond, Martin na wengine wakitathmini picha zilizopigwa
Crew ya I-View Media
Diamond akijiandaa kwa photoshoot
Martin na Diamond kwenye pozi




Picha kwa hisani ya thisisdiamond.com




