Breaking NUUUUUUUZ!!!.....:Azam FC yamuuza Ngassa kwa El Mereikh ya Sudan kwa Milioni 120
Baada ya kushindwa kufikia dau lililowekwa na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati (Yanga) la kumuuza kiungo wake, Haruna Niyonzima, timu ya El Mereikh ya Sudan imeamua umwaga dola 75,000 (Shs 120 Milioni ) kumchukua mshambuliaji, Mrisho Ngassa.
Habari za uhakika zilizoifikia Globu ya Jamii muda huu zimesema kuwa viongozi wa timu hizo mbili walifikia makubaliano hay oleo na tayari Ngassa ambaye kwa sasa yupo Uganda akishiriki michuano ya Chalenji amepewa taarifa hizo na kukubali kwenda huku Sudan mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.
Taarifa hizo zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Azam FC zilisema kuwa Ngassa alikuwa anaichezea Simba SC kwa mkopo pamoja na timu hiyo kufikia dau la sh Milioni 25 kabla ya kuanza kwa msimu wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Chanzo chetu kimesema kuwa maamuzi ya kumuuza Ngassa ni chanya zaidi kwani wamepita lengo lao la Dola za Kimarekani 50,000 (Sh milioni 80) za hapo awali. Ngassa kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji nyota katika mashindano ya Chalenji na sasa anawania kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao matano.
Awali, El Mereikh ilitaka kumsajili Niyonzima, hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Bin Kleb alisema kuwa waishindwa kukubaliana dau la timu hiyo (Dola 40,000) ni ndogo kulinganisha na thamani ya mchezaji mwenyewe.





