Share this Post

dailyvideo

IKULU YA SOMALIA YASHAMBULIWA


Wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia wameshambulia Ikulu ya Rais katika mji mkuu Mogadishu. Umoja wa mataifa unasema umefahamishwa kuwa rais wa nchi hiyo hakujeruhiwa na yu salama na kwamba shambulizi la wanamgambo hao lilitibuka.
Waziri wa mambo ya usalama wa nchi hiyo Abdi Karim Hussein, amesema baadhi ya washambuliaji wamefariki na wengine kukamatwa.
Kundi la Al- Shaabab linalopigana na utawala nchini humo limedai kuhusika na shambulio hilo na kusema makabiliano yangali yanaendelea.
Walianza mashambulizi yao, kwa kutumia gari lililokuwa na bomu ndani yake kwa kuliegesha kando ya ukuta na kisha kuanza kupigana ili kuweza kuingia ndani.
Milipuko mikubwa ilisikika pamoja na milio ya risasi.
Majeshi ya muungano wa Afrika yamekuwa yakipambana na wapiganaji hao na hata kuwafurusha kutoka mji mkuu Mogadishu. Hata hivyo bado wanadhibiti sehemu nyingi nje ya Mogadishu
CHANZO: BBC SWAHILI

Posted by Editor on 16:23. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for IKULU YA SOMALIA YASHAMBULIWA

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery