Share this Post

dailyvideo

. KUPITISHWA KWA SHERIA YA KUHARAMISHA USHOGA, UGANDA YANYIMWA DOLA 90 NA BENKI YA DUNIA ILIYOKUWA IMARISHE SEKTA YA AFYA.

Yoweri-Museveni RAIS YOWERI MUSEVEN.

BENKI ya dunia imesitisha mkopo wa dola milioni 90 kwa Uganda wa kuimarisha sekta ya afya kufuatia kupitishwa kwa sheria inayoharamisha ushoga na kutoa adhabu kali kwa watakaopatikana na hatia.
Hatua hiyo ya benki ya dunia haikutarajiwa na wengi kwani taasisi hiyo mara nyingi hujiepusha kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa ya nchi wanachama au kuhusiana na masuala kama haki za mashoga, kuepuka kuzishurutisha nchi wanachame wake 188.

Hata hivyo msemaji wa benki hiyo David Theis amesema katika barua pepe kuwa wamesitisha mradi huo wa kuboresha sekta ya afya ya Uganda hadi watakapoufanyia tathmini na kuhakikisha malengo yake ya maendeleo hayataathiriwa na sheria hiyo mpya ya kuharamisha ushoga.

Rais wa benki hiyo Jim Yong Kim amewatumia wafanyakazi wake barua akisema benki ya dunia inapinga ubaguzi na itawalinda wafanyakazi wake wote na kuongeza kupitishwa kwa sheria hiyo ya Uganda sio nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani ushoga umeharamishwa katika nchi 83 na zaidi ya nyingine 100 zinawabagua wanawake.

Mkopo ulikuwa uimarishe sekta ya afya
Licha ya kusimamishwa kwa mkopo huo wa dola milioni 90,benki ya dunia bado ina miradi mingine nchini Uganda ya kiasi cha dola bilioni 1.56. Mkopo huo ulitarajiwa kuidhinishwa hapo jana na ulipaswa kuangazia miradi ya kuboresha afya ya uzazi,afya ya watoto wachanga na uzazi wa mpango.

Kutiwa saini kwa sheria hiyo ya kuharamisha ushoga Uganda na Rais Yoweri Museveni mapema wiki hii kumeibua shutuma kali kutoka kwa nchi za magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Norway,Denmark na Uholanzi zimetangaza kuwa zitasitisha misaada kwa serikali ya Uganda kutokana na sheria hiyo na nchi nyingine wafadhili ikiwemo Marekani pia zimetishia kusitisha misaada na kutafakari upya uhusiano kati yao na Uganda.

Ghadhabu hiyo ya nchi za magharibi kuhusu kuharamishwa kwa ushoga ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha gerezani kwa watakaokutikana na hatia imeporomosha thamani ya shilingi ya Uganda na kusababisha Benki nchini humo kuingilia kati kwa siku mbili mfululizo.

Serikali ya Uganda haina wasiwasi
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amesema Uganda inaweza kujiendeleza bila ya misaada kutoka nchi za magharibi na kuongeza Uganda haina wasiwasi na hatua hizo kwani ni wakati kwa Afrika kupinga ukoloni, utumwa na ubabe kutoka magharibi.

Mwanaharakati ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kuwatetea mashoga nchini Uganda Frank Mugisha alikutana na maafisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington hapo jana kuomba usaidizi utakaowalinda mashoga.

Ofisi ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa umelaani kuchapishwa kwa majina ya watu wanaodaiwa kuwa mashoga nchini Uganda katika gazeti moja la udaku nchini humo na kuonya hatua hiyo inakiuka haki ya kuwa na faragha na kuonyesha wazi kuwa maisha ya mashoga yamo hatarini.

Kiongozi wa upinzani Uganda Kizza Besigye ameishutumu serikali kwa kutumia suala hilo kuwahadaa raia wa nchi hiyo ili wasiangalie masuala muhimu kama ufisadi au kuwepo kwa jeshi la Uganda Sudan Kusini.(E.L)

Posted by Editor on 09:29. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for . KUPITISHWA KWA SHERIA YA KUHARAMISHA USHOGA, UGANDA YANYIMWA DOLA 90 NA BENKI YA DUNIA ILIYOKUWA IMARISHE SEKTA YA AFYA.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery