Share this Post

dailyvideo

NORWAY YAIFUTIA UGANDA MSAADA


 
Raia wa Uganda akiwa aameshika bango, tayari kwa kushiriki katika maandamano ya kupinga sheria iliyowekwa ya kuvaa nguo fupi. 
Kampala.Serikali ya Norway imesitisha msaada wa kiasi cha Sh 20 bilioni  kwa Uganda baada ya Serikali ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kusaini muswada wa sheria dhidi ya   ndoa za jinsia moja.
Sheria hiyo iliwaudhi viongozi wa nchi za Magharibi, ikiwamo Marekani, ambayo Rais wake, Barack Obama alieleza kuwa inafaa kuangaliwa upya.
Rais Yoweri Museveni, ambaye  amekuwa mpinzani mkubwa wa  vitendo vya ushoga, alisaini sheria hiyo Jumatatu wiki hii.
 “Sheria hii mpya inapinga haki za msingi za binadamu na pia inakiuka katiba ya nchi hiyo (Uganda),’’ alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Borge Brende.
Aliongeza: “Tutazuia msaada wa Kroner 50 milioni (Sh 20 bilioni za Uganda) na tutaongeza jitihada zetu na nguvu zote na  ushirikiano katika masuala ya haki za binadamu   na kuhakikisha demokrasia inalindwa nchini Uganda.
Waziri huyo alitoa tamko hilo kupitia kwa msaidizi wa Balozi wa Norway nchini Uganda, Kyree Holm
“Rais (Museveni)  alisaini muswada huo ambao unatoa adhabu kali kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kufanya vitendo vya uhusiano wa jinsia moja, sheria ambayo inakiuka  misingi ya raia wa nchi yake,” alisema Holm.
Naye Mkurugenzi wa Sera za Nje  wa Umoja wa Ulaya (EU), Catherine Ashton alisema kwamba kilichofanyika Uganda ni ubabe kwani huwezi kutoa kifungo cha maisha kwa kuwa na uhusiano wa jinsia moja.
Muswada wa kupiga marufuku  uhusiano wa watu wa jinsia moja ulipitishwa Desemba mwaka jana na Bunge la Uganda baada ya mjadala mkali.
Miongoni mwa vipengele vya muswada huo, ni vile vinavyotoa amri ya kufungwa jela maisha kwa mtu atakayekutwa na hatia ya kuwa na uhusiano huo, ikiwa ni pamoja na wale wanaohamasisha na vitendo hivyo.
Hata hivyo, nchi za Magharibi ikiwamo Marekani zilikasirishwa  na hatua hiyo ya Uganda.

Rais Obama alitishia kuwa uhusiano wa Uganda na nchi yake utaharibika kutokana na hatua ya Rais Museveni kusaini muswada huo na kuufanya kuwa sheria.

Muungano wa vyama vya wapenzi wa jinsia moja nchini  Uganda umeazimia kuandaa sala ya pamoja ambayo wameiita ya amani ya kuiombea dua Serikali ya nchi yao baada ya kupitisha muswada huo kuwa sheria

Posted by Editor on 09:32. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for NORWAY YAIFUTIA UGANDA MSAADA

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery