Share this Post

dailyvideo

SKYLIGHT BAND WAFANYA UZINDUZI RASMI WA NYIMBO YAO MPYA YA KARIAKOO PAMOJA NA KUTAMBULISHA STUDIO YAO MPYA YA KUREKODIA MUZIKI.

Meneja  wa Band ya Skylight Aneth Kushaba akielezea kwa kina uzinduzi Rasmi wa wimbo wao Mpya unaokwenda kwa jina la Kariakoo ambapo uzinduzi huo uliambatana na Video pamoja na Audio. Pia ametambulisha Rasmi Studio ya kurekodi Muziki ambapo sasa nyimbo zao watakuwa wanafanyia katika Studio yao.

 Kutoka kushoto ni mmoja wa waimbaji wa Skylight Band Sam Mapenzi, wakatikati ni Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba pamoja na Mwimbaji mwengine wa Skylight Band Joniko Flower wakiwa wanazungumza na waandishi wa Habari na wadau mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa wimbo wao mpya wa Kariakoo pamoja na Kutambulisha Rasmi Studio yao

Meneja wa Skylight Band Aneth kushaba akitangaza rasmi ratiba zao za show ya Pasaka ambapo Tarehe 20/04/2014 watakuwa wanashow ya nguvu Mwanza Skylight Beach Resort (Jembe Beach) ambapo Watakao kata tiketi  kabla itakuwa ni Tsh 10,000 na watakao katia Getini itakuwa ni Tsh 15,000 Pia tarehe 27/04/2014 kutakuwa na Tamasha maalum la kutambulisha Nyimbo mpya na wanamuziki wapya Escape One ambapo panafanyika Show za kila Jumapili ,aliongeza kuwa kila siku ya Ijumaa Show huwa Thai Village Masaki.
Baadhi ya wanamuziki wa Band ya Skylight wakiwa wanafuatilia kwa umakini utambulisho huo wa wimbo wao mpya wa Kariakoo pamoja na Studio mpya ya kisasa ambayo itatumika kutengenezea nyimbo zao zote.
Baadhi ya wadau pamoja na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa umakini Utambulisho huo wa wimbo mpya wa Skylight Band Kariakoo pamoja na Kutambulisha Studio mpya ya Kurekodia Muziki.
 Studio Mpya ya Kisasa ya Skylight Band ambapo watakuwa wakirekodia nyimbo zao
 Muuandaji wa Muziki (Producer) Djobandjo akiwa ndani ya Studio za Skylight Band ambapo alikuwa anajiandaa kuwasikilizisha wadau pamoja na waandishi wa Habari nyimbo mpya ambayo wanaifanya sasa.
 Waimbaji wa Skylight Band wakiwa katika studio Maalum ya Kurekodia Muziki ambapo hapa walikuwa wakiimba wimbo wao mpya wa Kariakoo.
 Skylight Band wakiwa wanaimba Live wimbo wao mpya wa Kariakoo

Tazama hapa Video ya wimbo wa KariakooTaarifa kwa Vyombo vya Habari

Posted by Editor on 16:10. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for SKYLIGHT BAND WAFANYA UZINDUZI RASMI WA NYIMBO YAO MPYA YA KARIAKOO PAMOJA NA KUTAMBULISHA STUDIO YAO MPYA YA KUREKODIA MUZIKI.

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery