Stars yatuma salamu Zimbabwe
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
Na Sosthenes Nyoni,
Dar es Salaam. Timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars imetuma salamu Zimbabwe baada ya kuichapa Malawi
kwa bao 1-0 jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiungo wa Simba, Amri Kiemba
aliifungia Stars bao pekee dakika 36 akimalizia kazi nzuri ya Shomari
Kapombe, Kelvin Friday na Simon Msuva. Huo ni ushindi wa pili kwa kocha
Mart Nooij tangu alipopewa jukumu la kuinoa Stars mwanzoni mwa mwezi
huu.
Taifa Stars inajiandaa na mechi yake
ya marudiano dhidi ya Zimbabwe itakayopigwa Juni Mosi jijiniHarare
katika kutafuta kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2015.
Kikosi cha stars
Taifa Stars iliuanza mchezo huo kwa
kasi na dakika ya 16, Friday lililopaa juu kidogo ya lango la Malawi.
Kiemba naye alikosa bao dakika ya 20, baada ya shuti lake kupaa juu
kidogo ya lango la Malawi.
Kiemba alijirekebisha na dakika ya 36
aliifungia Stars bao la kuongoza kwa shuti baada ya pasi safi kati ya
Shomari Kapombe, Friday na Msuva. Stars walikwenda mapumziko wakiwa
mbele kwa bao hilo moja, lakini pamoja na kutengeneza nafasi kadhaa za
kufunga, washambuliaji wake walionekana kukosa umakini katika
umaliziaji.
Kocha wa Stars, Nooij aliwapumzisha Msuva na Himid Mao na kuwaingiza Ramadhani Singano na Haruna Chanongo kipindi cha pili.
Malawi nusura wasawazishe bao dakika ya 60, wakati Chimango Kaira aliposhindwa kumalizia pasi nzuri ya Bashir Maunde.
Chanzo: Mwananchi