Share this Post

dailyvideo

Hatimaye Cameroon waelekea Brazil

Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Hatimaye The Indomitable Lions ya Cameroun waabiri ndege ya Brazil
Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.
Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia kiwango cha fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ni idadi gani walichoongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.

BBC

Posted by Editor on 20:00. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Hatimaye Cameroon waelekea Brazil

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery