KIPI NI KIPI? Uzazi, elimu au kazi?
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Sasa je nini ukweli kuhusu umri unaofaa kwa wanawake kupata watoto?
Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa mwaka 2013 nchini Uingereza, wanawake bila shaka hawapaswi kupoteza matumai ikiwa umepita umri wa kuzaa yaani kati ya miaka 25-40
'Umri upi unafaa?'

Utafiti huo unasema kuwa wale ambao hawapati watoto katika mwaka wa kwanza, takriban nusu yao watajifungua katika mwaka wao wa pili wa ndoa.
Idadi ya wanawake ambao wanapatwa na shida ya kushika mimba ni asilimia kumi nchini Uingereza. Bi Allsopp, anahoji ikiwa ni sawa kwa wanawake kuweka kando mpango wa elimu ya juu zaidi ili kupatia kipaombele swala la uzazi? Nini maoni yako?
Tunajua vyema kuwa uwezo wa mwanamke kushika mimba hupungua kadri umri wake unapoendelea kukua.
Lakini wataalamu wanasema kwamba sio rahisi kama inavyodhaniwa.
Wanawake wengine wanapata ugumu kushika mimba hata wakiwa na umri wa miaka 20 kuelekea juu wakati wengine wakigundua kuwa hawana tatizo la kuzaa hata wakiwa na zaidi ya miaka 40.
'Mfumo wa maisha'

Mfumo wa maisha ukiwa moja ya sababu hizo, lakini wakati mwingi huwa ni vigumu kueleza kwa nini mwanamke hawezi kushika mimba.
Watoto wasichana huzaliwa wakiwa na mayai mengi, karibu milioni moja. Lakini wanapovunja ungo huwa ni mayai 400,000 pekee ambayo huwa yamebakia mwilini.
Mayai haya huendelea kupungua mwanamke anapokuwa. Takriban mayai 1,000 hupotea kila mwazi.
Wataalamu wa afya wanasema ni bora kwa wanawake kujaribu kupata watoto wanapokuwa wachanga wa umri kuanzia miaka 20 hadi thelathini na tano. Ujauzito wao hautakuwa na changamoto nyingi na pia itakuwa rahisi kwao kujifungua na pia kufurahia watoto wao.
Lakini mfumo wa siku hizi wa maisha hauwezi kuruhusu hilo kufanyika.
Elimu ya juu, kazi na kumsaka 'Mr Right' au mwanamume unayemuona kuwa sawa kwa maisha na ndoa naye. Yote haya yana maana kuwa mwanamke anaweza tu kupata mtoto akiwa na umri wa miaka 30 kuelekea juu.
Wanawake wanaofika umri wa miaka 40 wanakabiliwa na tisho la mimba kutoka, au hata kutoshika hiyo mimba na pia watoto wanaozaliwa katika umri huo huwa na matatizo mengi ya kiafya.
