Yafahamu mataifa ya Afrika yanayotumia wanyama na ndege kama nembo ya taifa (Wanyama wa Taifa)
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
TANZANIA
Nchi ya Tanzania inatumia mnyama Twiga kama alama ya taifa/nembo na kwa hiyo analindwa na sheria.
Ingawa
tangazo la kipekee huweza kutolewa na Rais, huwa kawaida, kuua Twiga
kunaweza kukusababisha kufungwa jela. Twiga ni mnyama mpole mwenye
shingo ndefu inayowakilisha uwezo wa kuona mbali tukiwa bado tunaangalia
yaliyopita na ya sasa. Twiga pia anawakumbusha Watanzania kutumia nguvu
zao na kuwa tayari kujipanga kimwili, kiakili na kiroho kama twiga.
Angola
Nchi
ya Angola ina mnyama wa taifa na ndege wa taifa, huitwa Magnificent
Frigatebird na swala. Ndege huyu ameitwa hivi kutokana na hadithi ya
usawa ya - the Man O'War.
Ameitwa
hivyo kutokana na ukimya wakati wa kuruka, kasi na tabia yake ya kuiba
nyama kutoka mwa ndege wengine. Swala mweusi nchini Angola wako katika
hatari.
Lesotho
Mnyama
wa taifa wa nchi ya Lesotho ni faru mweusi. Makazi hatari kwa mnyama
huyu yalikuwa ni mashariki na katikati mwa Africa. Faru sasa wana maisha
magumu nchini Afrika Kusini kutokana na uhitaji wa pembe zao kwa madai
ya dawa za asili ya kichina.
Hivi
karibuni raia mmoja wa kigeni amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa
kosa la uwindaji haramu wa faru. Faru anachukuliwa kuwa na kinga ya
asili kutokana na ngozi yao nyembamba, ukubwa na pembe – kuwafnya kuwa
alama ya taifa.
Madagascar
Mnyama
wa taifa la Madagascar ni komba bukini, mbegu ya pekee ambayo
inapatikana katika kisiwa hicho cha barani Africa pekee. Komba bukini
wanaaminika kuwa wamekuwepo kisiwani hapo kwa miaka 65 million
iliyopita.
Wanyama
hawa wapo katika hatari ya kutoweka kutokana na tabia ya uwindani na
usafirishaji. Komba bukini hutumiwa sana na watu wanaosoma nadharia ya
mabadiliko kutokana na upekee wake.
Nigeria na Ghana
Tai
ni chaguo lingine maarufu, kwa nchi kadhaa kuchagua tai au tofauti yake
kuwa mnyama wa taifa. Hii inajumuisha nchi za Misri na Mauritius
hutumia tai wa rangi ya dhahabu, Nigeria na Ghana tai na nchi za Sudan
Kusini na Zambia hutumia tai-samaki wa kiafrika.
Tai
hujulikana kutokana na kasi yao na size, na nafasi yao ya uwindaji
katika ulimwengu wa ndege, hii huwafanya kutumika kama alama ya taifa.
Tai wa kike katika vizazi vyote huwa wakubwa zaidi kuliko tai wa kiume.
Ni alama ya taifa katika mataifa mengi kama vile Marekani, Ujerumani,
Albania, Hispania na mengineyo mengi.
Rwanda
Mnyama
wa taifa la Rwanda ni cdhui wa kiafrika. Chui huyu wa kiafrika
anajulikana kutokana na vidoti (mara nyingi hukosewa na kuitwa madoa).
Pia upo uwepo wa chui weusi.
Hupenda
kuishi katika maeneo ya milimani, misitu mikubwa ya mvua na sehemu ya
jangwa na hupenda kula chakula kingi pale wanapokipata. Wako katika
hatari ya kutoweka kutokana na ushindani na binadamu juu ya makazi na
majangili na huwa wakiwindwa.
Ivory Coast
Nchi ya Ivory Coast (sanjari na nchi za Kenya, Msumbiji na Afrika Kusini) wamechagua tembo wa kiafrika kuwa mnyama wa taifa.
Tembo
wa kiafrika ni mnyama mkubwa zaidi miongoni mwa wanyama duniani.
Wanachukuliwa kuwa miongoni mwa wanyama wenye akili ulimwenguni.
DRC
Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo ina aina ya pekee ya mnyama wa taifa
ajulikanaye kama okapi. Wanyama hawa wadogo wanaonekana kufanana na
twiga (mnyama anayeonekana kufanana naye sana) na pundamilia (kutokana
na marakaraka).
Okapi
wana ndimi ndefu za rangi ya bluu, ndimi hizi ni ndefu na huzitumia
kuangalia masikio yao. Wanyama hawa hawapo katika hatari yoyote, ingawa,
wanahitaji sehemu kubwa ya kususurika/kuzurura na sasa wanatishiwa
kuwindwa na kuharibiwa kwa makazi yao.
Ethiopia na Liberia
Simba
ni chaguo katika mataifa haya kuwa mnyama wa taifa tofauti na tai
mkubwa. Simba ni mnyama mkubwa anayeishi katika jamii yap aka baada ya
tiger, wana upeo na ni muwindaji mzuri katika maeneo yao ya asili.
Wanaweza kupatikana katika maeneo ya jangwa la sahara barani Africa na
bara la Asia.
Simba
inasemekana kuwa adimu huku ikisemwa kuwa, namba yao inapungua katika
maeneo ya mashariki na kusini mwa kwa 30-50% katika kipindi cha miaka 20
iliyopita kutokana na kuiliwa makazi yao na binadamu. Vizazi kadhaa vya
simba vimekuwepo tangu zamani sana. Nchi nyingine ambazo humtumia simba
kama alama ya taifa ni Ubelgiji, Luxemborg, Uholanzi, Singapore na
nyinginezo.
Botswana
Mnyama
wa taifa la Botswana ni pundamilia, marakaraka ya farasi. Pundamilia
hutofautiana kwa sababu ya marakaraka yao na sababu kwamba hawakuwahi
kufugwa.
Kuna
nadharia kadhaa zinazoeleza ni kwa nini pundamilia wana rangi ya namna
hiyo.wanapatikana zaidi katika maeneo ya mashariki na kusini mwa Africa.
Algeria
Taifa lililopo kaskazini mwa Africa Algeria limemchagua mnyama mbweha kuwa alama ya taifa.
Mbweha
wanaotumika kama alama ya kitaifa ya Algeria ni wadogo sana
kulinganisha na mbweha wengine duniani na huweza kutambulik kutokana na
masikio yake makubwa.
