Share this Post

dailyvideo

Kutoka Gaza: Maafa Watu 100 wauawa katika mashambulizi



Idadi ya wlaiofariki imefika 100
Idadi ya watu waliofariki katika mashambulizi yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza, katika siku nne zilizopita, imefika watu miamoja.
Israel imefanya mashambulizi mengi sana nchini Israel tangu kuanza operesheni yake dhidi ya Gaza Jumanne kukabiliana na mashambulizi kutoka Gaza.
Hata hivyo wapiganaji katika ukanda wa Gaza nao hawajasitisha mashambulizi yao dhidi ya Israel.
Msemaji katika wizara ya afya eneo la Gaza, amesema kuwa katika mashambulizi yaliyofanyika hivi punde, wanaume wawili wameuawa katika eneo la Bureij.
Mashambulizi yamefanywa kwa kutumia roketi, ambazo zililipua kituo cha mafuta Kusini mwa Israel katika mji wa Ashdod.

Kwa mara ya kwanza makombora yamerushwa nchini Israel kutoka Lebanon
Watu watatu wamejeruhiwa vibaya, mmoja akiwa hali mahututi katika shambulizi ambalo limesemekana kuwa baya zaidi dhidi ya Israel tangu mgogoro huu kuanza.
Roketi zimekuwa zikirushwa Kaskazini mwa Israel kutoka Lebanon kwa mara ya kwanza katika mzozo huu.
Jeshi la Lebanon limesema linajaribu kuchunguza kujua nani aliyefanya mashambulizi hayo.
Marekani imejitolea kusaidia pande hizo kwenye mgogoro kufikia mwafaka kutuliza vita.
Ripoti zinasema kuwa pamoja na wale waliouawa, watu 675 wengi wakiwa raia , wamejeruhiwa.
Hata hivyo Israel inasema kuwa ni wapiganaji pekee waliouawa.
BBC NEWS
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Posted by Editor on 17:20. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for Kutoka Gaza: Maafa Watu 100 wauawa katika mashambulizi

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery