Share this Post

dailyvideo

TUKIO KATIKA PICHA HIVI NDIVYO JINSI MSANII DIAMOND ALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE UWANJA WA NDEGE DAR NA MASHABIKI WAKE ALIPOTOKA MAREKANI JANA


Tarehe 10/7/2014 ni siku ambayo Star wa muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania Diamond Platnumz, ambaye anachafua anga la muziki kwa sasa kwa utunzi na uimbaji wake alitua katika Uwanja wa Ndege Mwal. Jurius Nyerere, mnamo mishare ya saa nne na nusu za usiku akitokea nchini Marekani ambapo alikua huko kushiriki katika Tuzo kubwa Dunia  BET awards, ambazo hufanyika kila mwaka, Diamond alikua katika kategori ya Best African Act ambayo ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria.
Watanzania wenye moyo wa Upendo na Kizalendo walijitokeza katika viwanja vya ndege kumpokea Msanii huyo, wakiwa na mabango makubwa kabisa yenye maneno ya kuashiria ushujaa aliouonyesha Diamond katika muziki na kuipeperusha vyema  Bendera ya Tanzania katika muziki, Uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere, uligubikwa na Kelele za Furaha na Sauti zilisikika zikiimba wimbo wa Mdogomdogo ikiwa ni mapenzi ya dhati kabisa kwa Diamond kwa kutuwakilisha vema na kurejea salama, hakika kazi ya muziki wetu kwa sasa inaonekana.


Diamond baada ya kufika aliwashukuru wote waliofika kumpokea na kusema kuwa safari yake ilikua nzuri na amejifunza vitu vingi sana pia amekutana na watu wengi na tutaraji mengine mengi na mazuri katika muziki wetu, na kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kabisa kwa watanzania kuipokea vema video yake mpya ya mdogomdogo, imekua ikifanya vizuri sana na hata youtube imekuwa na views wengi kwa muda mchache








































 









Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Posted by Editor on 10:17. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0

0 comments for TUKIO KATIKA PICHA HIVI NDIVYO JINSI MSANII DIAMOND ALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE UWANJA WA NDEGE DAR NA MASHABIKI WAKE ALIPOTOKA MAREKANI JANA

Post a Comment

Recent Entries

Recent Comments

Photo Gallery