NEYMAR KUIKOSOA UJERUMANI NUSU FAINALI, AKIMBIZWA HOSPITALI, SCOLARI ATHIBITISHA!
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399
NYOTA
wa Brazil, Neymar, ataikosa mechi ya nusu fainali baina ya wenyeji
dhidi ya Ujerumani jumanne ijayo, hii ni kwa mujibu wa kocha, Luiz
Felipe Scolari.
Taifa
mwenyeji limefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa
mabao 2-1 mjini Fortaleza, lakini nyota wake alitolewa nje kwa machela
dakika tatu kabla ya mechi kumalizika na amekimbizwa hospitali baada ya
mechi kumalizika kutokana na kupata majeruhi ya mgongo.
Neymar
amekuwa akijikaza kuimarika katika mechi zote za Brazil kutokana na
majeruhi ya goti, lakini alifaulu kuanza katika mechi zote.
Neymar akiwa amelala chini baada ya kupata majeruhi ya mgongo dakika tatu kabla ya mechi kumalizika. Hapa machela: Neymar akitolewa nje ya uwanja kwa machela, huku akiwaacha mashabiki na taifa zima likiwa katika hofu kubwa.
Kusoma zaidi habari hii bofya www.bkmtata.blogspot.com