SOMA BARUA KUTOKA KWA MUME WA FLORA MBASHA KWENDA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA YOTE HAPA
Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

"Mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo
vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro
kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu
kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9
na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya
mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa
mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango
kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa
kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi
kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3
mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu
katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa
fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION
ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na
mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti
maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!
Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu
ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie
njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??
Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi
kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash
zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku
ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na
aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna
nini hapo??
Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!
Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda
katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia
hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya
forest hill!!
Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na
serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo
ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!
Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia
watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!!
Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!!
Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu
arudi hotelini kingsway!!
Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale
hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa
chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala
wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera
hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata
namba ya dereva taxi ninayo!!
Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea
lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda
ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala
hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!!
Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe
mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point
hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu
jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa
kunitishia jela miaka 30!!!
Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu
kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako
but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena,
nitakushinda.!!
Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini
kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha
zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia
mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea
mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje
watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini
aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto
watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na
mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa
dhambi ambayo hawajaitenda
Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi
embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka
makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata
ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi
tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja
ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso,
dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko
hapa!!!
Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu
hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi
ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!
Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na
wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini
kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe
Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili
wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata
mkewangu??
Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi
mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku
mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini
kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya
tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe
kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi
kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea
kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!
Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali
mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu
atatuhukumu kwa dhambi hii!!
Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya
habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji
wote tuta loose!!
Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza
nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka
shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta
maumivu makali kwenye ukoo!!
Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu,
nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na
kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!
Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa
sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole
kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu
kuwa wewe ni nyoka!!
Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na
nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora
nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!
Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata
wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga
magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje
familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na
kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..
Chanzo Vijimambo Blog


jamani hadi huruma, lkn huyu dada ni zaid ya shetan.
pole sana pia hongera sana kwa kuwa na msimamo mzuri. nimependa neno lako "mtapambana lakini UTASHINDA" tunakuombea kwa mungu azidi kukupa nguvu na ulinzi katika hili. usikate tamaa kumpigania mkeo kwani kaingia pasipo kutarajia. shetani anaguvu na mbinu nyingi sana. zidi kuomba ili upate nguvu za kuirudisha familia yako. flora ni mkeo ambaye mungu na wazazi walikukabidhi, ni wako sio wa kwajima. pigana na UTASHINDA. mtashindana lakini siku zote ushindi ni kwa yule amtegemeae mungu pekee kwani hata akiagua hatfika chini mungu humuokoa.muokoe mkeo flora pia msamehe kwani amezingirwa na shetani gwajima. UTASHINDA EMMANUELI MBASHA.